• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Kenya yapata mkopo wa bilioni 20 za kufadhili mradi wa umeme

    (GMT+08:00) 2017-03-28 18:16:39

    Wakenya ambao hadi sasa huduma za umeme haijafika majumbani mwao wana imani ya kuipata huduma hiyo baada ya serikali kupata mkopo.

    Kenya imepata mkopo wa shilingi bilioni-20 kutoka kwa benki ya uwekezaji ya bara ulaya kufadhili mpango wa kuwaunganishia umeme Wakenya zaidi.

    Pesa hizo zitaiwezesha kampuni ya Kenya Power kuwaunganishia umeme wateja laki 3 wapya.

    Benki ya uwekezaji ya bara ulaya imetoa mkopo wa shilingi bilioni 6.6; serikali ya ufaransa itachangia shilingi bilioni-9.9 huku muungano wa ulaya ukiipa Kenya ruzuku ya shilingi bilioni 3.3. mkopo huo utakaotozwa riba ya chini ya asilimia 2 na kulipwa katika muda wa miaka 20 .

    Utafiti uliotekelezwa na taasisi ya usimamizi wa maswala ya wafanyikazi umeonyesha kwamba sekta ya umma huenda ikwaajiri watu zaidi mwaka huu ikilinganishwa na sekta ya kibinafsi.

    Ripoti hiyo pia inasema kuwa kampuni nyingi katika sekta ya kibinafsi hazinuii kuongeza mishahara kutokana na viwango duni vya ukuaji uchumi.

    Na hatimaye wataalamu wa kilimo wamebuni teknolojia kumi mpya kushughulikia hasara za mavuno huku nchi hii ikitafuta mbinu za kupunguza uharibifu wa chakula.

    Wataalamu wanaoenelea kwamba kupunguza hasara hiyo ni njia bora zaidi ya kuhakikisha kuna chakula cha kutosha nchini na barani Afrika.

    Wakulima pia wamehimizwa kuhakikisha wanakausha nafaka zao vyema ili kupunguza visa vya kuathiriwa na sumu ya aflatoxin

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako