• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Benki ya Rwanda yapiga marufuku vituo vipya vya kubadilisha fedha za kigeni

    (GMT+08:00) 2017-03-28 18:16:54

    Benki ya taifa ya Rwanda imetangaza marufuku ya utoaji wa leseni kwa vituo vipya va ubadilishanaji fedha .

    Hatua hii itahakikisha kuwepo kwa ustawi wa mzunguko wa fedha na kuipa uhai sarafu ya nchi hiyo.

    John Rwangombwa gavana wa Benki kuu ya Rwanda amesema marufuku hiyo itawekwa kwa mda ili kuhakikisha oparesheni ya fedha inawekewa sheria mpya.

    Aidha vituo vya kubadilisha fedha za kigeni vya hapo awali vimetakiwa kuongeza mtaji wake hadi rwf 50 milioni kutoka kwa milioni 20.

    Vituo hivo sasa vitalazimishwa kuwa na vifaa vya kisasa vya kazi kwa ajili ya kuwepo kwa uwazi wa sheria za usalama wa taifa kuhusu fedha hatua inayonegwa kupunguza visa vya fedha bandia zinazotumika kufadhili ugaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako