• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda;Benki ya dunia yapongeza juhudi za ushirikiano wa sekta binafsi na serikali Rwanda

    (GMT+08:00) 2017-03-28 18:17:10

    Rwanda imepongezwa kwa juhudi zake katika ushirikiano wa sekta binafsi na serikali licha ya changamoto kadha zinazochipuka.

    Kwa mujibu wa ripoti ya ushirikiano huo,ukosefu wa miradi endelevu katika pande hizo mbili imekuwa kikwazo kikuu lakini katika miaka 5 iliyopita wadau wa serikali na sekta binafsi wamepiga hatua.

    Shymala Shukla Mtaalamu wa masuala ya uchumi amesema Rwanda inatakiwa kuweka mikakati bora ya uwekezaji ili kushawishi wawekezaji kutoka nje.

    Mwaka jana sheria mpya ya ushirikiano huo,imetoa maelezo muhimu ya utekelezaji na usimamizi.

    Wahandisi wametakiwa kuhakikisha wanapendekeza miradi ya maendeleo ya millennia chini ya kipengee cha 4 cha katiba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako