Kampuni kubwa ya usindikaji wa nyama nchini Brazil JBS imeanza tena uzalishaji hapo jana katika matawi yake 33 kati ya 36, ikiwa ni siku 10 baada ya kutokea kashfa mbaya iliyosababisha nchi kadhaa kuzuia bidhaa za nyama kutoka nchi hiyo.
Wakati sekta ya nyama nchini Brazil ikiwa bado inayumba kutokana na kashfa hiyo, matawi 33 ya kampuni ya JBS yalianza tena uzalishaji lakini kwa uwezo mdogo.
Takwimu rasmi zilizotolewa na Brazil zimesema, usafirishaji wa nyama ulishuka kutoka dola milioni 62.2 za kimarekani kwa siku wiki moja kabla ya kasfa hiyo na kufikia dola miliono 50.5 wiki iliyopita.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |