• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taifa Stars yaichakaza Intamba Murugamba ya Burundi

    (GMT+08:00) 2017-03-29 09:31:42

    Timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, imeiwasha Burundi, maarufu kama Intamba Murugamba, Bao 2-1 kwenye mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyochezwa jana uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

    Wakicheza bila ya nahodha wao Mbwana Samatta, Stars waliongoza 1-0 hadi mapumziko kwa bao la Simon Msuva aliefunga dakika ya 22.

    Burundi walisawazisha bao hilo dakika ya 53 kwa bao la mchezaji wa Simba ya Dar es Salaam Laudit Mavugo lakini dakika ya 77 Mbaraka Yussuf, aliifungia Taifa Stars hadi mwisho wa mchezo Taifa Stars iliibuka mshindi.

    Huu ni ushindi wa pili kwa Stars kwenye mechi ya pili baada ya wiki iliyopita kuiwasha Botswana, maarufu kama The Zebras, 'Pundamilia', Bao 2-0 pia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako