• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwanja wa Shanghai Shenhua wateketea kwa moto

    (GMT+08:00) 2017-03-29 09:33:56

    Klabu iliyovunja rekodi ya usajili kwa kumfanya Carlos Tevez kuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani, Shanghai Shenhua ambayo inashiriki ligi kuu ya nchini China jana imejikuta katika wakati mgumu baada ya sehemu kubwa ya uwanja wake kuteketea kwa moto.

    Moto mkubwa na moshi ulizigaa ukionekana kuendelea kusambaa katika uwanja huo wenye uwezo wa kubeba jumla ya watu 33,000 asubuhi ya jana jumanne hivyo kupelekea uwezekano wa klabu hiyo kucheza mchezo wake unaofuata katika viwanja vingine.

    Hata hivyo taarifa zilizotoka zimethibitisha kuwa hakuna mtu aliyeumia katika tukio hilo la moto huku shirika la zima moto likifanikiwa kuuzima moto huo. Mamlaka za mji mdogo wa Hongkou wanachunguza chanzo cha moto huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako