• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Olimpiki: Bodi ya Olympic ya Kenya (NOCK) yakubali kufanya mabadiliko ya Katiba.

    (GMT+08:00) 2017-03-29 09:34:30

    Bodi ya Olimpiki ya Kenya (NOCK) jana Jumanne ilikubali kufanya mabadiliko ya katiba yake na wito kwa uchaguzi mpya mwezi Mei kama walivyotakiwa na Kamati ya Olimpiki duniani (IOC).

    uamuzi huo unakuja baada kushindwa kufikia makubalino mara mbili hapo awali na kupelekea kamati ya olimpiki duniani kuzuia malipo kwa bodi ya Olimpiki ya Kenya mapema mwezi huu.

    Mkuu wa bodi ya NOCK, Kipchoge Keino amesema kuwa bodi hiyo imefurahishwa kwa kufikia makubaliano hayo ya pamoja ili kuokoa nchi ya Kenya kutokufungiwa katika mashindano mbalimbali ya Olimpiki.

    IOC sasa itawasaidia kuandaa rasimu ya sheria mpya kufuatia kashfa ya rushwa na matibabu ya timu ya Kenya katika mashindano ya Olimpiki ya Rio nchini Brazil.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako