• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FIFA yamfungia Messi mechi 4 kwa utovu wa nidhamu.

    (GMT+08:00) 2017-03-29 09:36:56

     

    Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA jana limetangaza kumfungia mechi nne kapteni wa Argentina Lionel Messi kufuatia kosa alilolitenda Machi 24 wakati wa mchezo dhidi ya Chile, Messi amefungiwa kutokana na utovu wa nidhamu wa kumtolea lugha isiyo ya kiungwana refa wa mchezo huo.

    Mbali ya kifungo hicho, Messi amelimwa faini ya Pauni 8,100. Taarifa ya FIFA imedai Messi amevunja Kipengele cha 57 cha kanuni za nidhamu za FIFA kwa kumrushia matusi refa msaidizi.

    Mara baada ya adhabu hiyo kutangazwa, AFA, Chama cha Soka Argentina, kimetangaza kukata rufaa kuipinga. Messi amekosa mechi na Bolivia, pia atakosa mechi za kuelekea kombe la dunia dhidi ya Uruguay, Venezuela na Ecuador.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako