• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyakula na misaada ya dharura vyasambazwa kwa watu elfu 25 Syria

    (GMT+08:00) 2017-03-29 09:44:24

    Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw Farhan Haq amesema Umoja wa Mataifa, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu pamoja na Shirika la misaada la Syria wamewapatia vyakula na misaada ya dharura watu elfu 25 walioko maeneo ya vijijini ya Damascus.

    Bw Farhan Haq amesema msafara wa magari ya Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Shirika la hilari nyekundi la Syria zimesambaza vyakula na msaada wa dharura kwa watu elfu 25 wenye mahitaji makubwa katika maeneo ya Buldan, Damascus.

    Aidha, Shirika la misaada la Hilari nyekundu ya Syria limewapatia msaada watu elfu 84 walioko Talbiseh mkoani Homs.

    Bw Haq ameongeza kuwa misaada ya kibinadamu inatakiwa kufikishwa kwa watu wa Syria bila vizuizi, hasa kwa watu milioni tano walioko kwenye sehemu za mbali na zinazodhibitiwa na waasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako