• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yarefusha marufuku ya kutotoka nje usiku Mandera kutokana na mashambulizi ya kigaidi

    (GMT+08:00) 2017-03-29 09:54:52

    Serikali ya Kenya imerefusha marufuku ya kutotoka nje usiku katika eneo la Mandera kwa miezi mitatu zaidi kufuatia mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa na kundi la Shabaab katika eneo hilo kwenye mpaka na Somalia.

    Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Bw. Joseph Nkaissery amesema, marufuku hiyo inaanza kutekelezwa leo hadi Juni 28.

    Amri hiyo ilitolewa kwa mara ya kwanza Oktoba 27 mwaka 2016 baada ya wapiganaji wa Somalia kuwaua watu 12 katika hoteli moja na kusababisha wengine sita kujeruhiwa. Kamishna wa kaunti ya Mandera Bw. Fedrick Shisia amewataka wakazi wa huko kuendelea kutii marufuku hiyo mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako