• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dola milioni 255 zahitajika kuwasaidia watoto wanaokabiliwa na njaa

    (GMT+08:00) 2017-03-29 14:15:53

    Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema, watoto takriban milioni 1.4 nchini Nigeria, Somalia, Sudan Kusini na Yemen wako katika hatari ya kukabiliwa na njaa, na kuitaka jumuiya ya kimataifa ichangie dola za kimarekani milioni 255 ili kutatua hali hiyo.

    UNICEF pia imetahadharisha kuwa hatari ya njaa si kama tu iko katika nchi hizo nne.

    Shirika hilo limesema kutokana na vurugu, njaa na ukosefu wa maji, watu wanalazimika kukimbia makazi na kukimbia nchi, na kiwango cha utapiamlo pia kitaendelea kuongezeka katika nchi jirani.

    UNICEF pia imesema watoto waliokimbia makazi hawana huduma za afya na lishe, maji safi, au mazingira safi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako