• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jamii ya Wachina nchini Ufaransa yadai haki baada ya Mchina mmoja kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi

    (GMT+08:00) 2017-03-29 16:44:14

    Jamii ya Wachina nchini Ufaransa imeandamana hapo jana kaskazini mashariki mwa mji wa Paris ili kudai haki baada ya polisi wa Ufaransa kumuua kwa kumpiga risasi mwanaume wa Kichina nyumbani kwake siku ya jumapili.

    Mamia ya waandamanaji hao walikusanyika mbele ya kituo cha polisi jumanne usiku, ili kutoka heshima kwa mwanaume huyo aliyeuawa na kupinga matumizi ya nguvu yaliyofanywa na polisi.

    Liu, raia wa China mwenye miaka 56, aliuawa kwa kupigwa risasi jumapili usiku nyumbani kwake baada ya jirani yake kupiga simu polisi kuripoti ugomvi wa kifamilia. Polisi wanasema Liu alipigwa risasi baada ya kujaribu kumshambulia askari polisi kwa mkasi mara mlango ulipofunguliwa.

    Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Matthias Fekl amesema upelelezi umeanza baada ya tukio hilo, na ameahidi sheria zitaheshimiwa ili kupata ukweli wote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako