• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WFP yatoa mpango wa kusaidia China kuondoa njaa

    (GMT+08:00) 2017-03-29 17:37:09

    Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) leo hapa Beijing limetoa mpango wa kimkakati wa taifa la China wa mwaka 2017 hadi mwaka 2021, ambao unalenga kushirikiana na wizara ya kilimo ya China na taasisi nyingine kujenga dunia isiyo na njaa na kusukuma mbele lengo la maendeleo endelevu duniani.

    Kwa mujibu wa mpango huo, WFP itasaidia serikali ya China kuboresha lishe ya wanafunzi wa elimu ya lazima katika maeneo ya vijijini, kusaidia wakulima wadogowadogo wenye matatizo ya kiuchumi, na kuyaongezea uwezo wa kujihuisha maeneo yanayokumbwa na maafa kwa urahisi. Pia itaunga mkono China katika kubadilishana uzoefu na nchi nyingine zinazoendelea katika usalama wa chakula, lishe na kupunguza umaskini.

    Habari zinasema, bajeti ya mpango huo wa miaka mitano ni dola za Marekani milioni 29 ambayo itatolewa kwa serikali, makampuni na watu binafsi nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako