• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazitaka pande husika kusimamisha mchakato wa kuweka THAAD

    (GMT+08:00) 2017-03-29 18:19:52

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo hapa Beijing amesema, China inapinga Marekani kuweka mfumo wa kujilinda na makombora THAAD katika eneo la Asia Mashariki, na kuitaka nchi hiyo kusitisha mpango huo.

    Bw. Lu Kang amesema, China inashikilia msimamo kwamba suala la kuweka mfumo huo linahusiana na utulivu wa kimkakati kote duniani na uaminifu miongoni mwa nchi kubwa, ambalo linapaswa kushughulikiwa kwa makini. Ameongeza kuwa, nchi mbalimbali zinapozingatia maslahi yao ya kiusalama, zinapaswa kuheshimu ufuatiliaji wa nchi nyingine juu ya mambo ya usalama, kufuata kanuni ya kulinda utulivu ya kimkakati duniani na kutoathiri usalama wa nchi zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako