• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: CBK inatarajia ukuaji wa mikopo katika makampuni kuimarika mwezi Aprili

    (GMT+08:00) 2017-03-29 19:19:04

    Maafisa katika sekta ya benki wanatarajia ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi kuanza kuimarika mwezi ujao.

    Mwezi Aprili ndiyo terehe ya mwisho ya benki za biashara kuwasilisha mifumo ya biashara upya kwa ajili ya ukuaji endelevu.

    Gavana wa Benki Kuu ya Kenya Patrick Njoroge amesema kwamba anatarajia mwaka hadi mwaka ukuaji wa matumizi wa mikopo na sekta binafsi ufike karibu asilimia 5.5 kuanzia mwezi ujao, na kupanda hadi asilimia 10 mwishoni mwa mwaka.

    Ukuaji wa mikopo katika sekta binafsi imetulia kwa asilimia 4.5 tangu Desemba 2016 baada ya kushuka kutoka asilimia 17 mwezi Desemba mwaka 2015.

    Benki lazima ziridhishe maafisa katika sekta ya benki kwamba kwamba mifumo yao mipya ya biashara itastahimili kuongezeka kwa ushindani miongoni mwa udhibiti udhibiti mkali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako