• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Rais wa Tanzania  atoa agizo la kufanya ukaguzi maalum kwenye sekta ya madini

    (GMT+08:00) 2017-03-29 19:19:34

    Rais wa Tanzania John Magufuli ameagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) kufanya ukaguzi maalum kwenye sekta ya madini ili kufichua mapengo ambayo yamekuwa yakisababisha serikali kupoteza kile wanapaswa kupata katika ukusanyaji wa mapato.

    Rais amasema ingawa nchi imebarikiwa na maliasili, ambayo ni pamoja na madini, wananchi wengi hawajapata kufaidika kwa sababu ya viongozi wasio waaminifu na wawekezaji wasioaminika.

    Dr Magufuli alitoa agizo hili jana, wakati alipokea ripoti ya Ukaguzi wa mwaka wa 2015/16 na baada ya spika wa Bunge, Bw Job Ndugai, kuahidi kuunda kamati ya bunge kuchunguza kama Tanzania imekuwa ikifaidika na sekta ya madini.

    Kulingana na Bw Ndugai, serikali imeendelea kupoteza mapato mengi katika sekta ya madini na kupitia misamaha ya kodi iliyoondolewa kwa wawekezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako