• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Brazil yawa taifa la kwanza kufuzu fainali za Kombe la Dunia

    (GMT+08:00) 2017-03-30 08:55:51

    Brazil imekuwa taifa la kwanza kufuzu katika fainali za Kombe la Dunia ambazo zitachezwa nchini Urusi mwaka ujao.

    Taifa hilo lilifuzu baada ya kuilaza Paraguay mabao 3-0, huku Argentina na Uruguay wakishindwa. Hii ina maana kwamba sasa Brazil haiweza kumaliza chini ya nafasi nne miongoni mwa mataifa ya Amerika Kusini, ambapo mataifa ya kwanza manne ndiyo hufuzu. Brazil waliwashinda Paraguay kupitia mabao ya mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, nyota wa Barcelona Neymar na mchezaji wa Real Madrid Marcelo.Neymar pia alipoteza mkwaju wa penalti.

    Brazil kwa sasa wana alama tisa mbele ya Colombia ambao wanashikilia nafasi ya pili.Huo ulikuwa ushindi wa nane kwa Brazil chini ya Tite. Paraguay, wao wako chini ya nne bora, zikiwa zimesalia mechi nne kuchezwa. Argentina wanakabiliwa na kibarua kufuzu baada ya kushindwa 2-0 na Bolivia na kushuka hadi nambari tano, alama moja nyuma ya Chile.

    Uruguay, waliochapwa 2-1 na Peru mjini Lima Jumanne, wanashika nafasi ya tatu. Taifa litakalomaliza nafasi ya tano litacheza mechi mbili za muondoano nyumbani na ugenini dhidi ya taifa kutoka Oceania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako