• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwanja wa ndege wa Madeira wapewa jina la Cristiano Ronaldo

    (GMT+08:00) 2017-03-30 09:37:35

    Moja kati ya vitu ambavyo vinaingia katika historia ya maisha ya nyota wa soka wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid Cristiano Ronaldo ni uwanja wa ndege wa kimataifa wa Madeira kubadilishwa jina na kupewa jina lake. Ronaldo jana alikwenda Madeira kuhudhuria sherehe za ubadilishwaji wa jina la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Madeira na kuitwa jina lake kwa heshima, sherehe ambayo imehudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo mashabiki. Cristiano Ronaldo alizaliwa 1985 Funchal Madeira nchini Ureno hivyo maamuzi ya uwanja wa ndege kupewa jina lake, yamekuja kutokana na kupewa heshima kutokana na jitihada zake ambazo amezifanya katika mchezo wa soka na jina lake kuitangaza vizuri Madeira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako