• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi wa mfuko wa dhamana ya elimu wa China wazinufaisha nchi kumi za Afrika

    (GMT+08:00) 2017-03-30 09:56:14

    Habari kutoka Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO imesema mradi wa mfuko wa dhamana ya elimu wa China umepata mafanikio katika kutoa mafunzo kwa walimu hodari wa Afrika, na idadi ya nchi za Afrika zinazonufaika na mradi huo imefikia kumi katika awamu yake ya pili.

    Katika mwaka 2012, serikali ya China na UNESCO zimesaini makubaliano ya mfumo wa dhamana yenye thamani ya dola milioni nane za kimarekani, ili kuunga mkono maendeleo ya elimu barani Afrika, hasa katika sekta ya kutoa mafunzo kwa walimu.

    Baada ya awamu ya kwanza ya mradi huo kumalizika na kupata mafanikio, serikali ya China imeongeza dola milioni nne za kimarekani na kurefusha mradi huo kwa miaka miwili. Licha ya Jamhuri ya Congo, Coate d'Ivoire, DRC, Ethiopia, Liberia, Namibia, Tanzania na Uganda, nchi nyingine mbili Togo na Zambia zitanufaika na mradi huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako