• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Safari za moja kwa moja za ndege kati Nairobi na Mogadishu Somalia zarejelewa.

    (GMT+08:00) 2017-03-30 18:54:42
    Safari za moja kwa moja za ndege kati Nairobi na Mogadishu Somalia zimerejelewa.

    Nege ya kwanza ikiwa na abiria 49 ilitua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Jumatano.

    Awali ndege zote za kibiashara kutoka Mogadishu zilitakiwa kwanza kutua mjini Wajir kwa ukaguzi wa kiusalama.

    Kurejeshwa kwa safari hizo kunafuatia ziara aliyofanya nchini Kenya rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo.

    Waziri wa usalama nchini Kenya Jospeh Nkaisery amesema wataendelea kuhakikisha ndege zote kutoka Somalia zinakaguliwa ili kudumisha hadhi ya kimataifa ya kiusalama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako