• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Sameer Africa yatangaza hasara ya shilingi milioni 877

    (GMT+08:00) 2017-03-30 18:55:22

    Kampuni ya kutengeneza magurudumu ya magari Sameer Africa imetangaza kwamba ilipata hasara ya shilingi milioni 877 kufuatia kufungwa kwa kiwanda chake mwaka jana.

    Imesema kwamba kupanga upya oparesheni zake na kufungwa kwa kiwanda kumeilazimu kutumbukia kwenye hasara.

    Sameer ilifunga kiwanda chake mwaka jana Agosti ikilalamikia mazingira mabaya ya kibiashara ikiwemo kuigizwa kwa magurudumu ya bei rahisi kutoka nchi za nje na kupanda kwa gharama ya uzalishaji.

    Sasa kampuni hiyo inapanga kuanza kuuza magurudumu yanayotengenezewa nje ya nchi, kukondisha kiwanda chake na kuwekeza kwenye ujenzi wa nyumba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako