• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serengeti Boys kuumana na Mali michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 17

    (GMT+08:00) 2017-03-31 08:48:07

    Kikosi cha timu ya soka ya taifa ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 cha Tanzania Serengeti Boys kitaumana na wenzao wa Mali katika mchezo wa kwanza wa michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo itakayofanyika nchini Gabon mwezi Mei.

    Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amethibitisha kuhusiana na ratiba ya timu ya Serengeti Boys ambayo kwa sasa iko mkoani Kagera kwa ziara ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Burundi.

    Hivi karibuni, FIFA ilitangaza kuifungia Mali katika soka ya Kimataifa kutokana na Serikali ya nchi hiyo kuingilia masuala ya soka hatua ambayo ingeiondoa Mali katika mchuano hiyo jambo ambalo huenda lingeweka unafuu kwa Serengeti Boys.

    Kurejeshwa kwa mali kunamaamisha kuwa sasa katika kundi B, Serengeti Boys bado itaendelea kuwa na timu za Mali, Niger na Angola.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako