• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Simba yasaliwa na siku chache kupigwa mnada kwa nyasi zake bandia

    (GMT+08:00) 2017-03-31 08:51:40

    Moja kati ya habari kubwa iliyokuwa ikijadiliwa na wapenda soka Tanzania jana ni kuhusiana na nyasi bandia za timu ya Simba kuwa zitapigwa mnada na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kutokana na kushindwa kuzilipia kodi bandarini, Simba waliomba msamaha wa kodi lakini imeshindikana.

    Hata hivyo kuna taarifa pia zilizotolewa baadae kuwa mtanzania Mbwana Samatta aliyewahi kucheza Simba ambaye kwa sasa anaichezea KRC Genk ya Ubelgiji amezilipia kodi, lakini ukurasa rasmi wa msemaji wa Simba Haji Manara na TRA unasema Samatta hajalipia kodi nyasi hizo. Ukweli wa taarifa rasmi ni kuwa Simba wameongezewa muda wa siku 14 wazilipie kodi nyasi zao hizo bandia ambazo wanampango wa kuziweka katika uwanja wao wa mazoezi wa Bunju, katika siku 14 walizopewa Simba tayari zimebakia siku mbili pekee.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako