• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNICEF yasema watoto wengi wanakabiliwa na utapiamlo na magonjwa Somalia

    (GMT+08:00) 2017-03-31 10:24:40

    Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema, watoto wengi zaidi nchini Somalia wanakumbwa na utapiamlo mkali na magonjwa ya kipindupindu na kuhara, kutokana na ukosefu wa chakula.

    Watoto zaidi ya 35,400 wenye utapiamlo mkali walipewa matibabu katika mamia ya vituo vya liche nchini humo mwezi wa Januari na Februari. Idadi hiyo imeongezeka kwa asilimia 58 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho.

    Wagonjwa zaidi ya 18,400 wa kipindupindu na kuhara wameripotiwa tangu mwanzo wa mwaka huu, wengi wao wakiwa ni watoto.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako