• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga kauli ya spika wa Bunge la Ulaya kuhusu uwekezaji wa China barani Afrika

    (GMT+08:00) 2017-03-31 19:13:21

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema, hakuna nadharia ya "ukoloni" katika mtazamo wa diplomasia ya China, na kwamba nchi za Ulaya ndizo zilifanya uvamizi na utawala wa kikoloni katika nchi za Afrika.

    Lu Kang amesema hayo kufuatia kauli iliyotolewa na spika wa Bunge la Ulaya Antonio Tajani kuwa Afrika inaweza kuwa koloni la China. Bw. Lu Kang amesisitiza kuwa, ukoloni wa Ulaya barani Afrika ni chanzo cha umaskini, machafuko na migongano inayoendelea barani humo. Pia amesema msaada wa China kwa Afrika unalenga kuzisaidia nchi za Afrika kutoka kujipatia uhuru wa kisiasa hadi kujitegemea kiuchumi, na unakaribishwa na watu wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako