• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Huduma ya PesaLink yazidisha ushindani mkali wa huduma za kuhamisha pesa nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2017-03-31 20:00:53
    Huduma mpya ya kuhamisha pesa ijulikanayo PesaLink imeendelea kuizidisha ushindani mkali wa huduma za kuhamisha pesa nchini Kenya. Wachambuzi wa mambo ya fedha wamesema huduma hiyo huenda ikaipa MPESA na njia zingine za kuhamisha pesa ushindani mkubwa hasa wakati huu ambapo watu wamezoea njia za kielektroniki za kutuma na kupokea hela.

    Tayari wateja milioni mbili ambao hutumia huduma za benki wamejisajili kutumia huduma ya PesaLink, ambayo inamilikiwa na Chama cha Wamiliki wa Mabenki nchini (KBA). Huduma hiyo ilianzishwa miezi miwili iliyopita na kampuni ya kiteknolojia ya Integrated Payment Services Limited (IPSL), inayomilikiwa na KBA.

    Jumla ya benki 22 ambazo zimeidhinishwa na Benki Kuu nchini (CBK) zinatumia huduma hiyo kuwezesha kuhamishwa kwa pesa kutoka kwa benki moja hadi nyingine.

    PesaLink inapatikana kwa takriban benki tano na wateja wanaweza kuhamisha pesa kutoka benki moja hadi nyingine na kupokelewa papo hapo katika upande mwingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako