• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Wakenya waendelea kupongeza bajeti ya serikali

    (GMT+08:00) 2017-03-31 20:02:32

    Wakenya wameendelea kupongeza bajeti ya serikali iliyosomwa jana bungeni baada ya waziri wa fedha Bw. Henry Rotich kupendekeza ushuru unaotozwa mahindi na ngano upunguzwe. Hii inamaanisha kuwa wakenya sasa wataweza kupika mlo wao wa ugali bila kidhibiti cha bei. Bw Rotich amesema hatua hiyo imelenga kuwapunguzia wananchi gharama ya maisha ambayo imekuwa ikipanda kwa kasi. Waziri amechukua hatua hiyo wakati ambapo ripoti zinaonyesha idadi kubwa ya wananchi wa kawaida wamepunguza kula ugali na badala yake kula chapati zaidi kutokana na bei ya juu ya unga wa mahindi isiyopungua Sh140 kwa pakiti ya kilo mbili. Hata hivyo, hatua hiyo haikufurahisha wabunge kutoka maeneo ambako kilimo cha mahindi ni tegemeo kubwa zaidi la mapato yao, kwani inamaanisha kuna uwezekano mkubwa bei ya mahindi itashuka na kuwanyima faida kubwa wakulima.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako