Kulingana na Shirikisho la Riadha duniani (IAAF), Kisorio alikimbia kilomita tano za mwisho pekee yake na kukamilisha umbali huo wa kilomita 42 kwa saa 2:07:32.
Mkenya Peter Some alikamilisha kwa kutumia saa 2:09:22, huku Mohamed Reda wa Morocco akitumia saa 2:09:50 na kukamilisha kitengo cha wanaume katika nafasi ya pili na ya tatu.
Kwa upande wa wanawake, Jepkosgei aliweza kunyakuwa taji hilo kwa kutumia saa 2:27:48. Akifuatiwa Winnie Jepkorir aliyetumia saa 2:27:52, Loice Kiptoo (2:28:39) na Nancy Koech (2:29:30) katika nafasi nne za kwanza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |