• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ligi kuu ya Uingereza (EPL) Chelsea washtushwa kwa kichapo, Arsenal yalazimishwa sare na Man City, Liverpool yaitandika Everton

    (GMT+08:00) 2017-04-03 08:24:17
    Kipigo cha vinara wa EPL, Ligi Kuu England, Chelsea cha 2-1 jumamosi kutoka kwa Crystal Palace kimewastua kiasi cha meneja wao kusema inabidi wapiganie ubingwa huo.

    Kipigo hicho na ushindi wa 2-0 wa Tottenham dhidi ya Burnley umefanya pengo la Chelsea ikiwa kileleni mwa ligi hiyo na timu inayoshika nafasi ya pili Tottenham Spurs sasa kuwa ni Pointi 7 huku mechi zikibaki 9 kwa timu hizo.

    Mechi nyingine Arsenal imelazimishwa sare na Manchester City ya mabao 2-2. Arsenal walipata bao la kuongoza katika dakika ya 40 lililofungwa na Theo Walcott, Man City walisawazisha mnamo dakika ya 42 kupitia Sergio Aguero. Man City waliongeza bao la pili kupitia Leroy Sane huku Arsenal wakisawazisha katika dakika ya 53 bao lililofungwa na Shkodran Mustafi.

    Nayo Liverpool, imeitandika Everton goli 3-1. EPL itarindima tena Jumanne na Jumatano kwa Timu zote 20 kuwa dimbani huku Big Mechi, itakuwa Jumatano Stamford Bridge wakati Vinara Chelsea wakiivaa Man City.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako