• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • La liga: Real Madrid yaichakaza Alaves 3-0, Barcelona

    (GMT+08:00) 2017-04-03 08:24:55

    Read Madrid imeendeleza ubabe wake wa soka baada ya kuichakaza Alaves kwa mabao 3-0 mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Bernabeu.

    Alikuwa Karim Benzema aliyefungua ukurasa wa magoli kwa upande wa Real Madrid katika dakika ya 31. Mabao mengine ya Madrid yalifungwa na Isco katika dakika ya 85 na Nacho dakika ya 88. Dakika ya 54 bao la Christiano Ronaldo lilikataliwa.

    Barcelona nayo yaitandika Granada kwa jumla ya magoli 4-1 kwenye mchezo uliochezwa katika uwanja wa Nuevo Los Carmenes. Luis Suarez akifunga bao la kwanza katika dakika ya 44. Dakika ya 64, Paco Alcacer alifunga bao la pili, wenyeji Granada walipata bao la kufutia machozi lililofungwa na Jeremie Boga, dakika ya 83 Matthieu Saunier alijifunga na kufanya Barcelona kuongoza kwa mabao 3-0, Neymar alikamilisha msumari wa mabao kwa Barcelona baada ya kufunga goli safi dakika ya 90.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako