• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuongeza kiwango cha waongeaji wa kichina sanifu kwa asilimia 80

    (GMT+08:00) 2017-04-03 18:27:35

    Kwa mujibu wa mpango uliotolewa na Wizara ya Elimu na Idara ya Lugha, China imepanga kuongeza kiwango cha raia wanaoongea kichina sanifu cha mandarin hadi asilimia 80 ifikapo mwaka 2020.

    Mpango huo unataka kuboresha uwezo wa waongeaji kichina sanifu miongoni mwa walimu, hususan walimu wapya, ambao wanalazimika kufikia vigezo vya taifa vya lugha sanifu kabla ya kuajiriwa mashuleni.

    Mpango pia umesisitiza mafunzo kwa walimu kutoka mikoa ya makabila madogo. Njia za kufundishia ikiwemo ufundishaji kupitia mtandao wa internet zitatumiwa kuhakikisha walimu wote wa makabila madogo wanaoongea kichina sanifu.

    Hivi sasa idadi ya waongeaji kichina sanifu ni zaidi ya asilimia 70, lakini bado kuna pengo kubwa kati ya mikoa tofauti na makundi ya watu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako