• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Tanzania na Ufaransa kufanya kikao cha uwekezaji

    (GMT+08:00) 2017-04-04 18:57:05

    Mabalozi wa Ufaransa wanaotumikia nchi hiyo barani Afrika, ni miongoni mwa washiriki 200 wa mkutano mkubwa wa kuonesha utayari wa taifa hilo katika kuchangia safari ya Tanzania kuelekea katika uchumi wa viwanda.

    Mkutano huo ambao pia kampuni 50 za Ufaransa zitashiriki zikiwamo kampuni kubwa kama Total, Airbus, Sogea Satom na Alstom, kutakuwa na majadiliano mbalimbali kati ya wafanyabiashara wa Ufaransa na Tanzania ili kuona wapi taifa hilo linaweza kushiriki katika uwekezaji.

    Taarifa ya kuwapo kwa mkutano huo ilitolewa na Balozi wa Ufaransa nchini, Malika Berak wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya Ufaransa inayoanza Jumatatu, Aprili 3 hadi 6, mwaka huu.

    Alisema Wiki ya Ufaransa ambayo itafanyika kwa mara ya kwanza nchini katika Makumbusho ya Taifa, imelenga kuimarisha uhusiano wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Ufaransa, ambao kwa sasa wanafanya biashara inayofikia Euro milioni 200 kwa mwaka huku anayeingiza sana akiwa ni Ufaransa.

    Aidha, wiki hiyo itakuwa na mazungumzo kati ya watendaji wa serikali, wafanyabiashara hao wa Ufaransa na wa hapa nyumbani, makongamano na maonesho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako