• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tetesi za Zlatan Ibrahimovic kuhamia LA Galaxy zazidi kuwa kubwa

    (GMT+08:00) 2017-04-05 08:24:46

    Nyota wa kimataifa wa Sweden ambaye anaichezea Man United ya England Zlatan Ibrahimovic kwa wiki kadhaa sasa amekuwa akihusishwa kuwa na mpango wa kujiunga na LA Galaxy ya Ligi Kuu Marekani, Zlatan hadi sasa ameichezea Man United michezo 41 na kuifungia magoli 26 akitoa usaidizi mara 9 katika mashindano yote.

    Uvumi wa nyota huyo kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kwenda kujiunga na LA Galaxy ya Marekani unazidi kuwa mkubwa baada ya nyota huyo kutosema chochote kuhusiana na msimamo wake licha ya kuwa kocha wa Man United Jose Mourinho mwezi uliopita alisema wanasubiri maamuzi ya Zlatan.

    Kituo cha TV cha Marekani kinachojihusisha na michezo FoxSports kimeandika habari kupitia ukurasa wake wa instagram wakisema Zlatan anakwenda Marekani huku picha yake inayoaminika ya kutengeneza ikionekana kavaa jezi za LA Galaxy.

    Kama taarifa za Zlatan Ibrahimovic zitakuwa za kweli kuwa ataondoka Man United mwisho wa msimu akiwa kamaliza mkataba wake, itakuwa kadumu na klabu hiyo mwaka mmoja tu toka ajiunge mwanzoni mwa msimu huu akitokea Paris Saint Germain ya Ufaransa kama mchezaji huru.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako