• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • David Moyes ajuta kwa kumtishia kumzaba kofi ripota mwanamke

    (GMT+08:00) 2017-04-05 08:25:37

    Kocha wa klabu ya Sunderland, David Moyes amesema anajutia sana kitendo cha kumtishia kumpiga kofi Ripota wa kituo cha BBC mwanadada Vicki Sparks. Baada ya mechi kumalizika dhidi ya Burnley Machi 18, Moyes aliulizwa na Vicki Sparks kama uwepo wa mmiliki wa klabu hiyo Ellis Short jukwaani umemuongezea wasiwasi zaidi.

    Moyes alijibu "Hapana".Lakini baada ya mahojiano, kocha huyo alimwambia Sparks "Unafaa kuzabwa kofi hata kama wewe ni mwanamke" na kumtaarifu awe "Makini" wakati ujao atakapokwenda.

    Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari Moyes amekiri kujutia kitendo hicho, na kusema ameongea na Ripota wa BBC, ambaye amekubali msamaha wake". .

    Hata hivyo baada ya waziri kivuli wa michezo wa Uingereza Rozena Allin-Khana kukitaka chama cha soka cha England FA kuingilia kati suala hilo imeripotiwa kuwa chama hicho sasa kitamuhoji Moyes.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako