• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfumo wa shindano la Top 8 kusalia kama ulivyo licha ya ligi kuu Kenya kupanuka

    (GMT+08:00) 2017-04-05 08:25:56

    AFISA mkuu mtendaji wa bodi inayoendesha ligi kuu nchini Kenya KPL, Jack Oguda amethibitisha kuwa mfumo wa shindano la Top 8 utasalia jinsi ulivyo licha ya ligi kuu kupanuka kutoka timu 16 hadi 18 kwa sasa.

    Kufuatia kupanuka kwa ligi kuu, kulizuka kwa tetesi kwamba pia shindano la Top 8 lingepanuliwa lakini uongozi wa KPL ambao hudhamini shindano hilo nao pia umesisitiza kuwa utasalia jinsi lilivyo.

    Shindano la Top 8 kila msimu huhusisha timu nane zilizomaliza katika nafasi hizo kwenye ligi kuu msimu uliotangulia ambapo bingwa hutuzwa donge nono la shilingi milioni moja za Kenya.

    Akizungumzia tetesi hizo, Oguda alithibitisha kuwa mfumo huo utasalia jinsi ulivyo ili kuhakikisha unakoleza ushindani. Muhoroni Youth ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo ila msimu huu hawatashiriki baada ya kumaliza msimu uliopita katika nafasi ya 10.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako