• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatangaza mswada wa kanuni ya kuwahimiza wananchi wote kusoma vitabu

    (GMT+08:00) 2017-04-05 18:18:28

    Ofisi ya mambo ya sheria katika Baraza la Serikali la China hivi karibuni ilikusanya maoni ya wananchi kuhusu mswada wa kanuni za kuwahimiza wananchi kusoma vitabu. Waraka huo umeeleza bayana kuwa, mashirika ya uchapishaji yanapaswa kuweka alama ya umri mwafaka wa wasomaji katika sehemu wazi kwenye vitabu vinavyochapishwa. Wataalamu wanaona kuwa, hatua hii inaonesha kuwa China inafanya juhudi za kuiweka kazi ya kuwahimiza wananchi kusoma katika mchakato wa kisheria. Caroline Nassoro ana maelezo zaidiā€¦

    Vitabu kama Simulizi za Andersen na Maswali Laki Moja vilisomwa na watoto kizazi baada ya kizazi, lakini hivi sasa havisomwi sana na watoto nchini China, ambapo vitabu vinavyohusisha mapenzi na mambo ya kigaidi vimevichukua nafasi na kupendwa zaidi. Bibi An anayekaa katika mtaa wa Men Tougou mjini Beijing anasema:

    "Hivi sasa wazazi hawana muda wa kutosha kukagua vitabu kwa vijana. Baadhi ya wazazi walilalamika kuwa wamegundua kuwa mambo mengi yaliyomo katika vitabu wanavyosoma watoto wao si mwafaka kwa vijana."

    Takwimu zimeonesha kuwa, mwaka 2015 wastani wa idadi ya vitabu vilivyochapishwa na kusomwa na wachina kwa mwaka ulikuwa 4.58, wakati huo huo idadi hiyo ilikuwa 11 nchini Korea Kusini, 20 nchini Ufaransa na 40 nchini Japan, hali inayoonesha kuwa bado kuna pengo kubwa kati ya China na nchi hizo. Ili kuwahimiza wananchi wote hususan vijana na watoto kusoma vitabu, kanuni hiyo itahimiza usomaji kufanyika kwa kufuata ngazi mbalimbali na kuendana na hali ya maendeleo ya kimwili na kimoyo ya vijana na watoto wenye umri tofauti.

    Mswada wa kanuni hiyo pia unahimiza maktaba za shule na mashirika ya utafiti wa kisayansi kutoa huduma za usomaji kwa wananchi wote, kuhimiza maduka kutangaza vitabu vizuri, na kuandaa shughuli mbalimbali za kueneza usomaji. Mkurugenzi wa Maabara ya Chuo Kikuu cha dawa na matibabu ya kichina ya Changchun Bw. Cui Wei anasema:

    "Hivi sasa jamii yetu imeingia katika kipindi cha kisasa cha upashaji wa habari, na wasomaji wanababaika na kushindwa kuchagua wakikabiliana na kiasi kikubwa cha vitabu vinavyochapishwa. Maktaba za vyuo vikuu zinapaswa kubeba jukumu la kuwaelekeza wanafunzi au kujulisha majarida au vitabu muhimu kwa jamii."

    Baadhi ya wachambuzi wanaona kuwa, hivi sasa idadi kubwa ya wachina wanasoma kwa kupitia mitandao wa Internet au vyombo vya mawasiliano kwenye mtandao wa Internet, na zaidi ya nusu ya watu wanasoma kwa kupitia Wechat, na wastani wa muda wa wachina wanasoma kwa kupitia njia ya Internet umefikia saa moja kwa siku, na kutimiza lengo la kusoma kila siku. Lakini wataalamu wanaona kuwa umaalumu wa usomaji kwa njia hiyo ni kusoma makala fupi, na kazi muhimu ni kuwahimiza wananchi kuwa na tabia ya kusoma kwa kina.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako