• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wasiopungua 6 wameuawa kwenye shambulizi dhidi ya mgahawa mjini Mogadishu

    (GMT+08:00) 2017-04-05 19:15:00

    Watu wasiopungua 6 wameuawa na wengine 10 wamejeruhiwa katika mlipuko dhidi ya mgahawa mjini Mogadishu karibu na majengo ya wizara mbili za Somalia.

    Ofisa wa polisi Ahmed Elmi amesema gari moja lililotegwa mabomu lililipuka katika mlango wa mgahawa ulioko mkabala na jengo la wizara ya michezo barabara ya Shangani, mjini Mogadishu. Makao makuu ya wizara ya usalama ya Somalia pia yako karibu na sehemu hiyo.

    Msemaji wa mamlaka ya eneo la Benadir Bw. Adbifitah Omar Halene pia amethibitisha shambulizi hilo, lakini amesema watu watano wameuawa. Amesema kikosi cha usalama kinatathimini hali ya mlipuko na wanatafuta mhusika wa shambulizi hilo. Mpaka sasa hakuna mtu aliyetaja kuhusika na shambulizi hilo.

    Mlipuko huo unatokea kabla ya hafla ya makabidhiano ya madaraka ya mawaziri wa serikali wiki hii.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako