• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: maendeleo ya miundombinu inasukuma juu deni la taifa hadi Sh3.76 trillion

    (GMT+08:00) 2017-04-05 19:19:51

    Jumla ya madeni nchini Kenya iliongezeka kwa Sh bilioni 608 katika kipindi cha miezi 12 hadi Desemba 2016.

    Takwimu mpya na Benki Kuu ya Kenya inaonyesha, kuongezeka kwa deni kumechangiwa na maendeleo ya miundombinu.

    Ripoti ya CBK inaonyesha thamani ya deni ilipanda hadi sh trilioni 3.763 kutoka Sh trilioni 3.155 mwaka uliopita .

    Fedha zilizokopwa ndani iliongezeka kwa asilimia 25.39 mwaka hadi mwaka hadi Sh trilioni 1.931 katika mwezi Desemba 2016 kutoka Sh trilioni 1.540, wakati madeni ya nje ilikua kwa asilimia 13.45 hadi Sh trilioni 1.83 kutoka Sh trilioni 1.62 mwaka mapema.

    Ripoti inaonyesha kuna kushuka kwa biashara ambayo ni tabia ya mwaka wa uchaguzi na bei duni ya bidhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako