• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania Samia akaribisha Ufaransa kujenga viwanda

    (GMT+08:00) 2017-04-05 19:20:38

    WAFANYABIASHARA wa Ufaransa wamekaribishwa kushiriki katika juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

    Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakati akifungua Wiki ya Ufaransa yenye lengo la kuonesha uwezo wa Ufaransa katika nyanja mbalimbali kuanzia nishati, uwezeshaji, na usafirishaji.

    Samia anasema Tanzania ni nchi yenye usalama na faida kwa mwekezaji hivyo wawe na uhakika na usalama wa mali ambayo wanaieleta kwa ajili ya kushirikiana na Watanzania.

    Akifungua maonesho ya kibiashara kati ya Ufaransa na Tanzania yanayofanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Makumbusho, Samia amewakaribisha wawekezaji hao kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbali hasa katika kilimo, nishati, utalii na usafiri.

    Aidha, Makamu wa Rais amewataka Watanzania serikalini, taasisi za umma na sekta binafsi kutumia wiki hiyo ya maonesho hayo ya kibiashara ambayo yataambatana na kongamano kubwa la kibiashara kati ya nchi hizo mbili kufanikisha sera ya viwanda nchini.

    Naye Balozi Ufaransa nchini, Malika Berak anasema lengo la Wiki ya Ufaransa ni kujenga na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili kwa manufaa ya wananchi wake.

    Aidha anasema watashirikiana na washiriki 200 kuonesha utayari wa taifa hilo la Ufaransa katika kuchangia safari ya Tanzania kuelekea katika uchumi wa viwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako