• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Arsenal yapata ushindi wa kwanza wa EPL baada ya siku 53 bila ushindi

    (GMT+08:00) 2017-04-06 08:47:19

    Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017 iliendelea jana usiku kwa michezo sita kuchezwa, miongoni mwa michezo hiyo ni ule kati ya Arsenal na West Ham United, licha ya watu wengi kufuatilia mechi ya Man City dhidi ya Chelsea iliyochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge na kumalizika kwa Chelsea kupata ushindi wa goli 2-1, lakini mchezo wa Arsenal ulikuwa na mvuto wake pia.

    Arsenal walifanikiwa kupata ushindi wao wa kwanza wa EPL baada ya siku 53 bila ushindi. Arsenal wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates walifanikiwa kupata ushindi wa goli 3-0 dhidi ya West Ham United ushindi ambao umeiwezesha kurudi nafasi ya tano na kuishusha Man United nafasi ya 6.

    Magoli ya Arsenal yalifungwa dakika ya 58 na Mesut Ozil, Theo Walcott alifunga goli la pili dakika ya 68 kabla ya Oliver Giroud kufunga goli la tatu lililoirudisha Arsenal katika nafasi ya 5.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako