• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Abdi Banda wa Simba aomba radhi kwa kumtwanga ngumi mchezaji mwenziwe

    (GMT+08:00) 2017-04-06 08:47:47

    Mlinzi wa kati wa Simba, Abdi Banda ameomba radhi kwa mashabiki wa soka nchini Tanzania kwa kitendo chake cha kumpiga ngumi, kiungo wa Kagera Sugar, George Kavilla Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

    Banda alikuwa mwenye bahati kwa kutotolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumtwanga ngumi Kavilla katika mchezo ambao Simba ililazwa 2-1 kutokana na tukio hilo kutoonwa na waamuzi.

    Baada ya siku mbili, Banda ameamua kuvunja ukimya na kuomba radhi kwa kitendo chake hicho. Katika kauli yake, Banda hajaeleza kwa uwazi kitu gani hasa alichokifanya na sababu za kufanya kitendo kile ambacho kilionekana dhahiri katika picha za video.

    Banda amesema alikutana na Kavilla baada ya mchezo kumuomba radhi ana kwa ana kwa kitendo kile, lakini ameona haitoshi bali pia awaombe radhi wapenzi wa soka kupitia vyombo vya Habari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako