• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Juventus yatinga fainali ya kombe la Copa Italia

    (GMT+08:00) 2017-04-06 08:48:15

    Klabu ya Juventus imetinga fainali ya kombe la Copa italia licha ya kufungwa na Napoli kwa mabao 3-2, katika mchezo wa nusu fainali ya pili.

    Juventus wamesonga mbele kwa jumla ya mabao 5-4, baada ya nusu fainali ya kwanza kushinda kwa mabao 3-1.

    Mchezo wa fainali utawakutanisha Juventus na Lazio na mchezo huo utapigwa june 2 mwaka huu katika dimba la Olimpico.

    Mshambuliajia wa Juventus raia wa Argentina Gonzalo Higuain ndie aliyeifungia mabao yote mawili timu yake huku mabao ya Napoli yakifungwa na mshambuliaji Marek Hamsik, Dries Mertens akifunga bao la pili huku Lorenzo Insigne akifunga bao la tatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako