• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hatma ya Sadio Mane kuendela kucheza katika msimu huu bado ni kitendawili

    (GMT+08:00) 2017-04-06 08:48:35

    Bado vichwa vya habari vinazidi kuchukua nafasi yake kuhusu hatma ya nyota wa kimataifa wa Senegal anayeichezea Liverpool ya England Sadio Mane kujua kama ataendelea kuitumikia timu yake ya Liverpool hivi karibuni au jeraha lake la goti litahitaji akae nje ya uwanja hadi mwisho wa msimu.

    Mtandao wa thisisanfield.com umeripoti kuwa uchunguzi bado unafanyika kuweza kufahamu kama Sadio Mane ataweza kurejea uwanjani mapema au atafanyiwa upasuaji na kukaa nje ya uwanja kwa kipindi chote cha msimu kilichosalia. Mane alitolewa uwanjani wakati wa mchezo uliokuwa na upinzani mkali katika jiji la Liverpool dhidi ya Everton siku ya Jumamosi, lakini jana zimetoka taarifa za kuwa nyota huyo yupo katika hatari ya kumalizia msimu huu nje ya uwanja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako