• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China akutana na viongozi wa Finland

    (GMT+08:00) 2017-04-06 10:48:48

    Rais Xi Jinping wa China jana kwa nyakati tofuati alikutana na waziri mkuu wa Finland Bw Juha Sipila, na spika wa bunge la Finland Bibi Maria Lohela mjini Helsinki.

    Akizungumza na waziri mkuu Bw. Sipila, rais Xi amesema China inapenda kushirikiana na Finland katika sekta mbalimbali, zikiwemo uvumbuzi wa teknolojia, uhifadhi wa mazingira, mambo ya Ncha Kaskazini, utalii na michezo. Pia amesema China inautakia Umoja wa Ulaya ustawi zaidi katika siku zijazo.

    Kwa upande wake Bw Sipila ameipongeza China kwa kazi zake kubwa kwenye mambo ya kimataifa, na kusema Finland inapenda kuhimiza ushirikiano kati ya nchi za Ulaya Kaskazini na China.

    Alipokutana na Spika wa bunge la Finland Bibi Maria Lohela, Rais Xi Jinping amesema China inaunga mkono mabunge ya nchi mbili kukamilisha utaratibu uliopo wa ushirikiano. Kwa upande wake Bi Lohela amesema Finland inapenda kuimarisha mawasiliano kati ya mabunge ya nchi hizo mbili, haswa kati ya wabunge vijana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako