• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Safari za Rwanda air Harare nchini Zimbabwe kukuza biashara

    (GMT+08:00) 2017-04-06 18:30:12

    Safari za ndege za moja kwa moja za shirika la Rwanda air kutoka Kigali hadi Harare nchini Zimbabwe zinatarajiwa kukuza biashara.

    Shirika hilo lilitatumia ndege yake aina ya B737-800NG Kalisimbi katika safari yake ya kwanza ikiwa na abiria 56..

    Safari ya Harare inafikisha 21 idadi ya maeneo zinakoenda ndege za shirika hilo.

    Sasa shirika hilo litafanya ziara mara nne kwa wiki lakini pia kuna safari zingine za kila siku kuelekea Lusaka Zambia.

    Wakati huo huo shirika la, RwandAir linatarajiwa kufanya ziara yake ya kwanza hadi London Uingereza baadaye mwezi Mei kabla ya ziara za Guangzhou -China na New York Marekani.

    Mwaka jana shirika hilo lilinunua ndege zake za kwanza aina ya A330-200 and A330-300 iki kuongeza uwezo wake wa kushindana kwenye soko la kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako