• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Kampuni ya Prime Cement Rwanda kufungua kiwanda cha saruji

    (GMT+08:00) 2017-04-06 18:30:57

    Kampuni ya Prime Cement, inapanga kufungua kiwanda cha saruji kwa gharama ya dola milioni 65 katika wilaya ya Musanze mkoa wa Kaskazini nchini Rwanda.

    Kampuni hiyo na ile ya FLSmidth ya Denmark ambayo inatengeneza vifaa vya viwanda vya saruji wamesaini makubaliano na ujenzi unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

    Gisele Bayigamba, ambaye ni mkurungezi wa kampuni ya Milbridge Holding, inayomiliki Prime Cement, amesema oparesheni kwenye kiwanda hicho kipya zitaanza baadaye mwaka 2018,

    Kitakapokamilika kiwanda hicho kinatarajiwa kuzalisha tani 700, 000 za saruji kila mwaka.

    Kampuni ya pekee ya kuzalisha saruji Cimerwa inazalisha tani 600,000 kila mwaka kwenye kiwanda chake kilichoko eneo la Ruzizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako