• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Viwavi jeshi watishia wakulima kaunti ya Taita Taveta nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2017-04-06 18:31:19

    Wakulima katika kaunti ya Taita Taveta nchini Kenya wana wasiwasi kufuatia kuzuka kwa viwavi jeshi ambao wamevamia mashamba yao na kuharibu mimea.

    Kundi la wataalam limepelekwa kwenye maeneo ya Njukini na Challa ambayo yanazalisha chakula kwa wingi.

    Gavana wa kaunti hiyo John Mruttu amewataka maafisa wa idara ya kilimo kushirikiana na wataalam ili kuaondoa hofu ya wadudu hao kwa wakulima.

    Viwavi hao ni sehemu ya kundi kubwa lililozuka katika nchi nyinginezo za Afrika.

    Wanasababisha uharibufu mkubwa kwa kula kila kitu chenye majani na hivyo ni tishio la usalama wa chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako