• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: DTB Tanzania yapata faida ya Sh31 bilioni

    (GMT+08:00) 2017-04-06 18:33:45

    Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Diamond Trust Tanzania (DTB),Viju Cherian amesema benki hiyo imepata faida ya Sh31 bilioni kwa mwaka 2016.

    Akizungumza jana Cherian alisema faida hiyo imeongezeka kwa asilimia 13.6 kutoka Sh27.3 bilioni ya mwaka 2015.

    Cherian alisema faida hiyo ni kubwa ikilinganishwa na ongezeko la kwenye sekta ya kibenki ambayo ni asilimia38 kwa mwaka 2016.

    Amesema ongezeko kubwa la faida kwa benki hiyo hasa wakati benki nyingine zikionekana kupata faida kwa kiasi kidogo, ni ishara kwamba wanaendelea kutoa huduma iliyo bora kwa wateja .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako