• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Naibu waziri mkuu wa China kufanya ziara nchini Russia

    (GMT+08:00) 2017-04-06 21:18:10

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo amesema, naibu waziri mkuu wa China Bw. Zhang Gaoli atafanya ziara nchini Russia, ambapo atabadilishana maoni na viongozi wa Russia kuhusu ushirikiano wa uwekezaji katika sekta za nishati, mambo ya fedha na sekta nyingine, ili kuhimiza ushirikiano kati ya pande hizo mbili kupata maendeleo mapya.

    Bibi Hua Chunying amesema ushirikiano wa uwekezaji na nishati ni sehemu muhimu ya ushirikiano kati ya China na Russia, pia ni sekta zilizopata mafanikio makubwa.

    Akiwa nchini Russia, Bw. Zhang Gaoli atahudhuria mkutano wa nne wa kamati ya ushirikiano wa uwekezaji kati ya China na Russia na mkutano wa wakuu wa kamati ya ushirikiano wa nishati kati ya China na Russia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako