• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Simba kuendeleza ushindi ili kugombea ubingwa

    (GMT+08:00) 2017-04-07 09:17:44

    Kocha wa Simba, Mussa Hassan 'Mgosi' amesema maandalizi ya mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC itakayochezwa Jumatatu Aprili 10, kwenye Uwanja wa CCM, Kirumba jijini Mwanza yanaendelea. Mgosi amesema kama watapoteza mchezo huo unaofuata, watakuwa hawana nafasi tena kwenye mbio za kusaka ubingwa wa msimu wa 2016/17 ambao unatarajiwa kumalizika ifikapo Mei 20, mwaka huu. Alisema wanaamini kuwa juhudi watakazofanya katika mechi hiyo zitafanikiwa, na hiyo inatokana na kila mchezaji "kuamka" na kutamani ushindi katika kila mechi.

    Hofu ya simba inafuatia kufungwa kwenye mecho dhidi ya timu ya Kagera Sugar. Mbali na Simba na Yanga kuchuana vikali kuwania taji hilo, vita nyingine katika ligi hiyo iko kwenye timu zinazopambana kujinasua kushuka daraja ambayo inahusisha Mbao FC, Ndanda FC, Toto Africans, Majimaji na JKT Ruvu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako